
ACT-Wazalendo, CCM wanavyonyosheana vidole uvunjifu amani Zanzibar
Unguja. Wakati Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi akieleza kuna kauli zimeanza kutolewa kuashiria uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Chama cha ACT-Wazalendo kimesema hakuwezi kuwa na amani kama hakuna haki. ACT-Wazalendo imesema licha ya viongozi wakuu kuhubiri amani, lakini matendo yanayotendeka yanaonesha hakuna nia ya dhati ya kuleta amani visiwani humo….