
Ujenzi Hospitali ya Mji wa Tarime wafika asilimia 90
Tarime. Serikali imetoa zaidi ya Sh900 milioni kwa ajili ya kukarabati na kuboresha miundombinu na majengo ya Hospitali ya Mji wa Tarime mkoani Mara kufuatia hospitali hiyo kuzidiwa na idadi ya wagonjwa wanaofika kupata huduma, ikilinganishwa na miundombinu iliyopo. Hospitali hiyo yenye uwezo wa kupokea na kuhudumia wagonjwa 150 kwa siku hivi sasa inapokea wagonjwa…