


WANANCHI JITOKEZE USHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
OfisaTarafa wa Nyaishozi Kelvin Berege amekabidhi Reflectors kwa maofisa Usafirishaji ( Boda Boda ) wa Kata zote ndani ya tarafa hiyo. Lengo ni kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha makundi mbalimbali ndani ya jamii, juu ya haki na wajibu wa mwananchi Kupiga/Kupigiwa Kura ifikapo Novemba 27 mwaka huu ambapo utafanyika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Mwandishi Mwanaspoti apewa cheti cha Heshima na Ubalozi wa Marekani
MWANDISHI wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited ambaye amekuwa akiandikia gazeti namba moja la michezo Tanzania, Mwanaspoti, Nevumba Abubakar, ameandika historia mpya katika taaluma yake baada ya kutunukiwa cheti cha heshima na Ubalozi wa Marekani, ikiwa ni sehemu ya kutambua umahiri wake kwenye utengenezaji wa maudhui ya kidigitali. Nevumba amekuwa mmoja wa vijana wachache waliobahatika…

UA YAANZISHA MITAALA YA UALIMU WA AMALI KUKABILIANA NA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA
Na Farida Mangube, Morogoro CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeanzisha mitaala mipya ya Ualimu wa Amali kwa ajili ya walimu wa shule za sekondari, ili kuwawezesha kufundisha masomo yenye mwelekeo wa kuwaandaa wanafunzi kujiajiri. Hatua hii inalenga kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana nchini. Akizungumza na waandishi wa habari mjini…

Utulivu watanda makanisa ya Askofu Gwajima
Dar/mikoani. Siku moja baada ya Serikali ya Tanzania kutangaza kulifuta Kanisa la Ufufuo na Uzima, hali imekuwa tofauti katika makanisa hayo mikoani kwa kila mmoja kusema lake. Uamuzi wa Serikali kulifuta kanisa hilo linalomilikiwa na Askofu Josephat Gwajima ni kile kilichoelezwa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa ni ukiukwaji wa Sheria ya Jumuiya…

KEDA (T) CO LTD YAGUSA JAMII KUJENGA DARAJA LA MBEZI-MSORWA-SHUNGUBWENI-BOZA
Mwamvua Mwinyi, Pwani KIWANDA cha KEDA (T) Ceramic Co. Ltd kimekamilisha ujenzi wa daraja katika Mto Msorwa, barabara ya Mbezi-Msorwa-Shungubweni-Boza, lililogharimu milioni 150 ili kuunganisha maeneo hayo. Mradi huo umetokana na mpango wa Kiwanda cha KEDA wa kurudisha fadhila kwa jamii pamoja na kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wananchi wanaonufaika…

Zile 10 za Chikola zapata ugumu
NYOTA wa Tabora United, Offen Chikola amekiri ameanza kupata shaka ya kutimiza ndoto zake za kufunga mabao 10 msimu huu ili kuweka rekodi binafsi katika Ligi Kuu Bara iliyopo ukingoni. Mshambuliaji huyo, alisema kwa sasa anakuna kichwa ili kuona anazitumia mechi nne zilizosalia za timu hiyo kufunga mabao matatu na kukamilisha hesabu ya mabao 10,…

Rais Samia awatembelea majeruhi ghorofa la Kariakoo, ampa matumaini mwanafunzi aliyenasa saa 24
Dar es Salaam. Mtapona kwa uwezo wa Mungu. Ndilo neno lililotawala kinywani mwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alipowatembelea na kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya jengo la ghorofa nne lililoporomoka Kariakoo. Jengo hilo, liliporomoka Jumamosi, Novemba 16, 2024 na mpaka sasa limesababisha vifo vya watu 20 na majeruhi zaidi ya 86, uharibifu wa…

90,000 wameyakimbia makazi yao katika saa 72 zilizopita, linaonya shirika la wakimbizi – Global Issues
Masaa tu mapema, UN Katibu Mkuu Antonio Guterresalionya ya Baraza la Usalama hiyo “Jehanamu inatoweka huko Lebanon” kando ya mstari wa utengano unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa, na ubadilishanaji wa moto zaidi katika “upeo, kina na ukali” kuliko hapo awali. Onyo hilo lilikuja wakati Rais wa Marekani Joe Biden aliwaambia viongozi wa dunia waliokusanyika katika…

Umoja wa Mataifa waguswa na ripoti ya kuongezeka mauaji ya raia nchini Burkina Faso
Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, imeguswa na ripoti za kuongezeka mauaji dhidi ya raia nchini Burkina Faso. Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa inaeleza hayo huku taarifa zikionyesha juu ya kuhusika jeshi na mamluki wa kigeni katika mauaji hayo. Kamishna Mkuu wa tume hiyo Volker Turk…