
PUMZI YA MOTO: Kutoka Neverkusen hadi Neverlosing
KAMA kuna hadithi tamu ya kuisimilia katika ulimwengu wa soka, basi ni hii ya muujiza wa kocha Xabi Alonso na klabu yake ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani. Baada ya miaka 120 ya uhai wao, Bayer Leverkusen wameshinda kwa mara ya kwanza taji la Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga).Timu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1904 ilikuwa imeshinda mataji mawili…