
Dereva basi la Kisire apandishwa kizimbani, asomewa makosa 22
Mwanza. Dereva wa basi la Kisire linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Sirari mkoani Mara, Adam Charles (30) amepandishwa kizimbani na kusomewa shtaka la kuendesha gari kwa mwendokasi na kusababisha majeruhi 21 na uharibifu wa mali. Katika kesi hiyo ya trafiki namba 188/2025, Charles ameitwa katika Mahakama ya Wilaya ya Magu mkoani humo mbele…