Mahakama yamkatalia Lissu kesi yake kusikilizwa mubashara

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, imeyakataa maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ya kesi yake kusikilizwa mubashara. Mahakama hiyo imesema kuwa ingawa ni msingi muhimu wa haki huru, kwamba haki inatakiwa siyo tu itendeke, bali  ionekane ikitendeka, lakini imesema kuwa hata hivyo hakuna kanuni zinazosimamia…

Read More

Lissu akwama tena kujinasua katika kesi ya uhaini

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amekwama tena kwenye jaribio la kujinasua katika kesi ya uhaini inayomkabili, baada ya Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam kutupilia mbali sababu nyingine ya pingamizi lake. Hii ni mara ya pili kwa Lissu jitihada zake za kumaliza kesi hiyo kwa mbinu…

Read More

DCMA, OlimpAfrica wafanya tamasha la muziki Zanzibar

CHUO cha Muziki (DCMA) kwa kushirikiana na Kituo cha OlimpAfrica, wamefanya tamasha la muziki lililopewa jina la Tutambue lililofanyika Dole, Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi. Katika tamasha hilo, Mkurugenzi wa Sanaa kutoka DCMA, Tryphone Evarist ametoa wito kwa wananchi kuacha kuamini kuwa muziki ni kazi isiyokuwa na maadili, huku akisisitiza kwamba hiyo ni…

Read More

Rais Mwinyi kununua bao la Mlandege, KMKM Sh5 milioni

KATIKA kutoa hamasa kwa timu za Zanzibar zinazoshiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema atanunua kila bao litakalofungwa na timu hizo kwa Sh5 milioni. Hayo yameelezwa jana Septemba 21, 2025 na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Fatma Hamad…

Read More

Polisi, TLS ngoma bado, Mwabukusi atoa angalizo

Dar es Salaam. Mvutano baina ya Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), umeendelea kuchukua sura mpya na sasa askari wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, wamezingira ofisi za chama hicho zilizopo Mikocheni, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi imeeleza makao makuu yake yamezingirwa na askari tangu asubuhi ya…

Read More