MGOMBEA UBUNGE CHATO KUSINI ACHANA MISTARI BONGO FREVA AKIOMBA KURA
Mgombea Ubunge Jimbo la Chato kusini,Paschal Lutandula, akichana mistari ya bongo dreva. ………… CHATO ZIKIWA zimesalia siku tano kufanyika Uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani nchini, mgombea Ubunge wa Jimbo la Chato kusini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paschal Lutandula, amelazimika kuchana mistari ya muziki wa kizazi jipya. Hatua hiyo ililenga kuomba kura kwa wananchi…
Mafyatu kumkaribisha Rais kuzindua kijiwe
Baada ya kuona kuwa inawezekana kumfyatua, sorry, kumchengua rahis hadi anazindua mangomangoma ya Hamnazoo, mafyatu tunakula mkakati kumkaribisha kuzindua kijiwe chetu cha ndumuu. Naona yule anatikisa kichwa kuwa rahis na vijiwe vya bangii, sorry, nimesema bangili wapi na wapi? Hamkumuona arap Rooter wa kwa njirani akijinoma na mchekeshaji kwa Joji Kichaka akiwatosa wake. Ama kweli…
Vijana wataka mambo manne wakiadhimisha siku yao
Dar es Salaam. Wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya amani Septemba 21, 2025, nchini Tanzania vijana wameeleza nafasi yao katika kudumisha amani, huku mambo manne yakijadiliwa katika kongamano la maadhimisho hayo. Septemba 21 ya kila mwaka dunia huadhimisha siku ya amani, hapa nchini maadhimisho hayo yameanza leo Septemba 18, 2025 kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali…
Changamoto sita za kimazingira Zanzibar, wadau wapendekeza hatua za kuchukua
Zanzibar. Zanzibar inakabiliwa na changamoto za kimazingira, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kina cha bahari, uvamizi wa maji ya chumvi, mmomonyoko wa fukwe, na hali mbaya ya hewa. Ofisa Uratibu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu, Omar Mohamed, ameeleza changamoto hizo leo Jumatatu, Machi 10, 2025 wakati wa warsha kuhusu uchumi rejelezi (Circular Economy)…
Serukamba afunga vibanda vya wafanyabiashara wasiolipa kodi Mafinga
Mufindi. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba ameagiza kufungwa kwa baadhi ya vibanda katika Soko Kuu la Mafinga lililopo katika halmashauri ya mji wa Mafinga, baada ya wafanyabiashara kushindwa kulipa kodi. Tayari baadhi ya vibanda hivyo vimezungushiwa utepe, ikiwa ishara ya kutoruhusu wafanyabiashara ambao hawajalipa kodi ya halmashauri kuendelea na shughuli zao hadi watakapolipa…
Mwinyi azindua ujenzi ‘flyover’ ya kwanza Zanzibar
Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amezindua ujenzi wa daraja la juu (flyover) la kwanza visiwani hapa, akisema ni sehemu ya mipango ya Serikali kuijenga Zanzibar kila upande. Dk Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Desemba 20, 2024 wakati akiweka jiwe la msingi wa daraja hilo eneo la Mwanakwerekwe ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka…
RC Mbeya aingilia kati sakata la Mdude, viongozi wa kimila…
Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk Juma Homera amesema tayari amelielekeza Jeshi la Polisi kuongeza jitihada za kuwatafuta wahusika waliomshambulia kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mdude Nyagali, huku akiahidi Sh5 milioni kwa atakayesaidia kumpata kada huyo alipo akiwa hai au amekufa. Hata hivyo, amesema pamoja na yeye kutojua tukio hilo, kwakuwa limetokea…
INEC: Jumla ya wapigakura waliojiandikisha ni milioni 37.65
Dar es Salaam. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imesema jumla ya watu milioni 37.65 wamejiandikisha kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba mwaka huu. INEC imefafanua kuwa kati ya wapigakura hao, milioni 36.65 wapo Tanzania Bara na 1,004,627 wapo Zanzibar. Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia…
Watu 12 mbaroni vurugu za wafugaji, wakulima Kilosa
Morogoro. Wakazi 12 wa Kijiji cha Malangali, Kata ya Tindiga wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro, wanashikiliwa polisi na wengine wanane wanaendelea kusakwa wakidaiwa kuhusika na vurugu za wafugaji na wakulima. Hata hivyo, Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishina wa Polisi (DCP), Mihayo Msikhela amesema jeshi hilo halitamvumilia yeyote atakaye vunja sheria….