
Mwili wa Sauli wapokelewa Mbeya, kuzikwa kesho
Mbeya. Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya mabasi ya Sauli, Solomon Mwalabila unatarajiwa kuzikwa kesho katika Kijiji cha Godima wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya. Mwili wa Mwalabila aliyefariki dunia Agosti 4, 2024 kwa ajali ya gari mkoani Pwani, umesafirishwa leo kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ukitokea Kibaha mkoani Pwani ulikokuwa umehifadhiwa…