Fidia kwa waliopisha mradi wa nyumba Chumbuni, mbioni

Unguja. Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC), limeanza mchakato wa ulipaji wa fidia kwa wananchi waliotoa vipando (mazao) yao kwa ajili ya kupisha mradi wa nyumba za makazi Chumbuni Unguja. Akizungumza katika kikao cha uhakiki na maelekezo kwa wahusika Machi 18, 2025, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Sultan Said Suleiman amewahakikishia wananchi hao kuwa hakuna atakayedhulumiwa…

Read More

RC Chongolo aiwakia halmashauri kwa kutowalipa wazabuni

Songwe. Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo ameiagiza halmashauri ya mji wa Tunduma kuwalipa wazabuni madai yao, yanayodaiwa kufika Sh1.8 bilioni tangu mwaka 2019, hali inayosababisha malalamiko mengi. Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Maendeleo ya Mkoa (RCC) kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26, Chongolo ameonyesha masikitiko yake…

Read More

Waumini wa kanisa la Gwajima washikiliwa na Polisi

Dar es Salaam. Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema wanawashikilia baadhi ya waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam. Kamanda Muliro amesema hayo leo Jumanne Juni 3, 2025 wakati akizungumza na Wasafi FM kuhusu kuwakamata waumini hao waliokaidi kanisa hilo…

Read More

Rais Samia asisitiza amani kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 2025

Unguja. Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali haitakubali atokee mtu yeyote kuvuruga amani na kusababisha mpasuko miongoni mwa wananchi hususani katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Amesema Taifa linapaswa kujifunza umuhimu wa amani kwa kuangalia nchi ambazo zimeikosa kwa kipindi kirefu, namna wananchi wake wanavyoathirika, jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya nchi. Rais…

Read More

Mtazamo tofauti uzito kuzidi kwenye mizani

Dar es Salaam. Wamiliki wa malori, madereva na wadau wa usafirishaji wamezungumzia changamoto za mizani kutoa taarifa tofauti za uzito, huku ubovu na kutofanyiwa ukarabati wa mara kwa mara vikitajwa. Hayo yameelezwa leo Machi 21, 2025 ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, kuwasimamisha kazi watumishi waliokuwa zamu katika mizani kutoka…

Read More