
Rais Samia awaweka kikaaangoni watendaji wa ardhi
Dar/Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan amewataka watendaji wa ardhi nchini kubadilika kwa sababu wananchi wanawalalamikia kwa rushwa, kujilimbikizia viwanja na kugawa kiwanja kimoja kwa watu wawili. Mbali na hilo, amewataka watumishi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), kubadilika kwa kutokuwa mvinyo uleule kwenye chupa mpya. Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu…