
Sh2.55 bilioni kutumika kuweka alama za barabarani mikoa yote
Dodoma. Serikali imetenga Sh2.55 bilioni katika mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya uwekaji alama na michoro ya usalama barabarani kwenye barabara kuu na za mikoa. Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya amesema hayo leo Agosti 30, 2024 alipojibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Latifa Khamis Juakali. Mbunge huyo amehoji Serikali imejipanga vipi katika…