WAFANYAKAZI WIZARA YA FEDHA WAPONGEZWA KWA KUJISIMAMIA VYEMA, KUTEKELEZA MAJUKUMU
*Wakumbushwa kutekeleza majukumu yao bila kuathiri afya zao Na Leandra Gabriel, Michuzi TV KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu Mwamba amewapongeza wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Taasisi zake kwa kujisimamia vyema katika utekelezaji wa majukumu kwa kufuata miongozo ya Serikali na kuwataka kuendelea kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miiko ya utumishi wa Umma…