
Maoni ya wadau nyongeza ya mshahara, kodi na elimu zatajwa
Dar es Salaam. Wadau wa sekta mbalimbali wameeleza maoni tofauti kuhusu ongezeko la kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma, lililotangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Ongezeko hili la asilimia 35.1, ambalo litaanza kutumika Julai mwaka huu 2025, linatarajiwa kuleta mabadiliko katika maisha ya watumishi wa umma, huku wengine wakiunga mkono hatua hiyo…