Wanawake 347 wakutwa na maambukizi saratani ya mlango wa kizazi Kagera
Kagera. Wanawake 347 mkoani hapa wamebainika kuwa na maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi baada ya kufanyiwa uchunguzi. Jumla ya wanawake 4,689 wamefanyiwa uchunguzi wa saratani hiyo mkoani Kagera. Akizungumza leo Jumatatu Aprili 22, 2024, katika maadhimisho ya chanjo Afrika yaliyofanyika Manispaa ya Bukoba, Mganga Mkuu wa Mkoa Kagera, Samwel Raizar amesema mkoa huo…