SMZ yapokea gawio la Sh10 bilioni kutoka PBZ
Unguja. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imepokea gawio la Sh10 bilioni kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ikiwa ni sehemu ya faida iliyopatikana kwa mwaka 2024. Kutokana na kazi zilifanywa na benki hiyo kwa mwaka huo, imefanikiwa kutengeneza faida ya Sh107 bilioni ambapo gawio lililotolewa litaingizwa moja kwa moja katika mfuko wa Serikali….