Kauli ya ‘tutawapoteza’ ya kigogo UVCCM moto
Mwanza/Kagera. Kauli ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Faris Buruhan ya kulitaka Jeshi la Polisi kutowatafuta vijana wanaotukana viongozi mtandaoni pindi watakapokuwa wamepotezwa, imezuia mjadala baada ya watu kuanza kukumbushia waliopotea kusipojulikana. Aprili 16, 2024, akizungumza na viongozi pamoja na vijana wakati wa ziara yake katika mji mdogo wa Rulenge Ngara mkoani…