‘Waliotumwa na afande’ wafikishwa mahakamani, wasomewa mashtaka mawili
Dodoma. Watu wanne wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Agosti 19, 2024 wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka mawili. Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Kanda Dodoma na kusomewa mashtaka ya kubaka kwa kikundi (gang rape) na kumwingilia kinyume na maumbile binti ambaye hakutajwa…