Aliyedaiwa kumuua mumewe afariki dunia baada ya kunywa sumu
Mufindi. Elizabeth Kihombo (46), mkazi wa Kijiji cha Ihefu kilichopo Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, aliyekuwa anatuhumiwa kwa kumuua mume wake, Philimon Lalika (49), amefariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibubu katika Hospitali ya Mji wa Mafinga. Tukio hilo limetokea Agosti 20, 2025 katika Kijiji cha Ihefu ambapo Elizabeth alimuua mume wake kwa kumchoma na kisu…