
Shule yenye wanafunzi 900 yalalama kutumia matundu saba ya vyoo
Kibaha. Shule ya Msingi Miembesaba iliyopo Manispaa ya Kibaha mkoani Pwani, inakabiliwa na upungufu wa matundu ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi, hivyo imewaangukia wadau ikiomba msaada wa kujengewa vyoo vya kisasa. Shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 944 na walimu 24, inahitaji matundu 39 ya vyoo, kwa sasa yapo saba pekee, jambo linasababisha msongamano…