Wasiojulikana wajeruhi, watoweka na Sh20 milioni
Same. Watu wasiojulikana wamemvamia na kumjeruhi kwa mapanga Yusto Mapande, mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro. Mapande alijeruhiwa alipokuwa akiingia nyumbani kwake akitokea kwenye biashara zake, pia ameporwa zaidi ya Sh20 milioni zilizokuwa kwenye gari lake. Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amethibitisha tukio hilo akisema limetokea jana Agosti 22,…