RC Babu asitisha matumizi ya ardhi eneo lenye mgogoro wa wakulima, wafugaji
Same. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesitisha kwa muda wa siku 14 shughuli zote za matumizi ya ardhi kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari 2,787 zilizopo katika Kijiji cha Marwa, Kata ya Ruvu, Wilaya ya Same mkoani humo, kufuatia mgogoro uliopo baina ya wakulima na wafugaji. Mkuu huyo wa mkoa amesema uamuzi huo…