
Mambo yameiva Dabi K’koo… Simba mtiti, Yanga mtiti
HUKO mtaani na katika mitandao ya kijamii kuna kelele nyingi za mashabiki wa soka wakitamani siku ziende haraka ili washuhudie Dabi ya Kariakoo ya kwanza kwa msimu wa 2025-2026. Ndiyo, Simba iliyomaliza nafasi ya pili Ligi Kuu Bara, italazimika kuvaana na Yanga iliyobeba mataji yote msimu uliopita kuanzia Ngao ya Jamii, Ligi Kuu hadi Kombe…