Polisi Morogoro yachunguza vifo viwili ikiwemo mtoto aliyejinyonga
Morogoro. Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linachunguza matukio mawili ya vifo yaliyotokea kwa nyakati tofauti, likiwemo la mwanaume aliyefariki dunia ghafla katika stendi ya mabasi ya Msamvu na mtoto wa miaka 12 anayedaiwa kujinyonga baada ya kukemewa na wazazi wake. Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 23, 2026 mjini hapa, Kamanda wa Polisi…