Ahly, Esperance fainali Mazembe, Mamelodi hoi
MAMBO ni moto. Miamba ya soka ya Afrika, Al Ahly na Esperance Tunis ndiyo itakayochuana kwenye mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu baada ya kuwasukuma nje wapinzani wao kwenye mechi za nusu fainali usiku wa Ijumaa. Al Ahly ilikuwa nyumbani huko Cairo, Misri kukipiga na TP Mazembe katika moja ya mechi…