Madiwani Ileje wamtaka DED ajitathimini usimamizi wa miradi

Ileje. Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Ileje mkoani Songwe limemtaka Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Nuru Kindamba ajitathimini katika usimamizi wa fedha za miradi zinazotolewa na Serikali Kuu. Hayo yamejiri leo Jumamosi Aprili 20, 2024 katika kikao cha Baraza la Madiwani baada ya madiwani hao kubaini miradi mingi ya maendeleo haijakamilika huku fedha…

Read More

Matola akiri ubingwa ni mgumu

Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola, amesema kupoteza tena mbele ya Yanga kumezidi kufanya safari ya ubingwa kuwa ngumu. Akizungumza baada ya dakika 90 za mchezo wa Kariakoo Dabi kumalizika, Matola amekiri wamepoteza nafasi ya ushindani kuwania ubingwa msimu huu, lakini haina maana kwamba ndio mwisho wa msimu kwani bado wana mechi nyingine zilizobaki. “Tulianza…

Read More

Sugu arejesha fomu akitaja vipaumbele vitatu kuimarisha Chadema Kanda ya Nyasa

Mbeya.  Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’ ametaja sababu zilizomvuta kuwania kiti hicho, huku akitaja vipaumbele vitatu kati ya 10 atakavyotekeleza akishinda. Sugu aliyewahi kuwa mbunge wa Mbeya Mjini anawania kiti hicho sambamba na mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter…

Read More

Gamondi achekelea kuichapa Simba, ausogelea ubingwa

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema licha ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba, amekiri kuwa haikuwa rahisi huku akiwamwagia sifa mastaa wake kwa kufanya kazi kwa usahihi. Gamondi amefunguka hayo muda mchache baada ya kukamilika kwa mchezo wa Kariakoo Dabi ambapo timu yake imefisha pointi 58 na kuendelea kujikita…

Read More

Dk Mwinyi awapa mbinu wahandisi utekelezaji miradi mikubwa

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema ili wahandisi wazawa wapewe miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali hawana budi kuungana kupata mitaji mikubwa.  Hata hivyo, amesema Serikali zote mbili zinaendelea kushirikisha taaluma ya uhandisi katika shughuli mbalimbali, ikiwamo kuweka mazingira yanayowawezesha kujiajiri. Dk Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Aprili 20, 2024 alipozindua taasisi ya wasanifu,…

Read More

Yanga yabakiza sita za ubingwa

Yanga imeendeleza ubabe kwa Simba baada ya kuichapa kwa mara ya pili ndani ya Ligi Kuu Bara katika msimu mmoja kutokana na kushinda mabao 2-1, leo Jumamosi, huku ikibakisha kushinda mechi sita kati ya nane ili kutetea ubingwa wake. Yanga imeibuka na ushindi huo kutokana na mabao ya Stephanie Aziz Ki dakika ya 20, akifunga…

Read More

Dk Nchimbi aibeba falsafa ya maridhiano ya Rais Samia

Songea. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amesema siasa ya vyama vingi si ugomvi, akiwataka wana-CCM na Watanzania kutoacha kuzungumza na kusalimiana, ili kujenga mshikamano wa Taifa.  Amewataka wanachama wa CCM kuishi katika misingi ya kutogombana, ili kutunza dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhimiza maridhiano na umoja wa kitaifa…

Read More

Vifo kutokana na mafuriko Mlimba vyafikia 49

Dar es Salaam. Msemaji wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema idadi ya vifo vilivyotokana na mafuriko katika Halmashauri ya Mlimba, mkoani Morogoro imefikia 49. Msemaji wa Serikali ameeleza hayo leo Aprili 20, 2024 jijini Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa juu ya hali ya mafuriko nchini na ratiba ya sherehe ya Muungano itakayofanyika Aprili 26, mwaka huu. …

Read More

Ujenzi nyumba za waathirika maporomoko ya Hanang waendelea

Arusha.Ujenzi wa nyumba 108 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya matope, mawe na magogo ya miti kutoka Mlima Hanang unaendelea katika eneo la Gidagamowd, Kata ya Mogitu.  Nyumba hizo zinajengwa kwa waathirika wa maafa hayo waliopoteza makazi yao na chache kwa wale wanaoishi kwenye mazingira hatarishi. Akizungumza na Mwananchi Digital, leo Aprili 20, 2024,…

Read More

Makowo wapewa gari la wagonjwa waliloomba serikalini 2021

Njombe. Wananchi wa Kata ya Makowo, Halmashauri ya Mji wa Njombe, wamepatiwa gari la kubeba wagonjwa litakalowapunguzia changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.  Akikabidhi gari hilo leo Jumamosi Aprili 20, 2024 Mbunge wa Njombe Mjini, Deo Mwanyika amesema mwaka 2021 aliomba hospitali hiyo ipatiwe vifaa tiba, wahudumu wa afya na gari la…

Read More