Saliboko ashika nafasi ya 71 Olimpiki
TANZANIA imepata pigo lingine katika Michezo ya Olimpiki ya Paris inayofanyika Ufaransa baada ya muogeleaji Collins Saliboko kushindwa kufuzu hatua inayofuata kwenye mashindano ya mita 100 freestyle, baada ya leo Jumanne Julai 30, 2024 kukamata nafasi ya 71 kati ya waogeleaji 79 alioshindana nao. Kabla ya hapo, jana Jumatatu Julai 29, 2024, mchezaji wa judo…