WATATU WAKAMATWA WAKISAFIRISHA ZAIDI YA KILO 420 ZA DAWA ZA KULEVYA.
WATU watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani Pwani wakikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Methemphetamine zenye uzito wa Kilogramu 424.84 pamoja na Heroin Hydrochloride gramu 158.24 Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Agness Ndanzi imewataja washtakiwa hao kuwa ni Rajabu Kisambwanda (42) mkazi…