WANANCHI WA LIWETA NA MASUKU MKOANI RUVUMA, WAISHUKURU TARURA KUKAMILISHA UJENZI WA DARAJA
Na Mwandishi Maalum,Ruvuma WANANCHI wa kijiji cha Liweta Halmashauri ya wilaya Songea mkoani Ruvuma,wameishukuru Wakala wa barabara za vijijini na mijini(TARURA)kwa kuwajengea daraja la kudumu katika mto Liweta linalounganisha kijiji hicho na Masuku na maeneo yao ya kilimo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema,awali walikuwa wakipata shida kubwa kupitia katika eneo hilo hasa wakati wa masika…