BARABARA ZOTE ZINAZOSIMAMIWA NA TANROADS ZILIZOATHIRIWA NA MVUA ZA EL-NINO ZINAFUNGULIWA KWA WAKATI-WAZIRI BASHUNGWA
Serikali inazifungua barabara zote zilizoathiriwa na mvua za El-Nino ambazo zimeendelea kunyesha kwa muda mrefu katika maeneo mbalimbali kote nchini na kuleta uharibifu wa miundombinu ya barabara. Licha ya uharibifu unaotokea Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kupitia kitengo cha dharura imekuwa ikirudisha mawasiliano kwenye maeneo ambayo mawasiliano yamekatika kutokana na uharibifu….