Wakongwe: Ni Dabi ya suluhu au sare
Mastaa waliowahi kuzichezea Simba na go Yanga wametoa utabiri wa mechi ya Kariakoo Dabi ya Ligi Kuu Bara inayopigwa kesho, Jumamosi, uwanjani Benjamin Mkapa, wengi wao wakiiona suluhu au sare. Mzunguko wa kwanza Simba ikiwa mwenyeji wa mchezo ilifungwa mabao 5-1, lakini pamoja na hilo mastaa hao hawaoni kama linaweza likajirudia. Mwanaspoti limefanya mahojiano na…