Mbivu, mbichi suala la kikokotoo kujulikana Mei Mosi
Dodoma. Serikali imesema suala la kanuni mpya ya kikokotoo cha pensheni ya wastaafu lina maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan na limeanza kufanyiwa kazi, majibu yatajulikana kwenye sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, jijini Arusha. Hayo yamesema leo Ijumaa Aprili 19, 2024 na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira…