Bakwata Mara waandaa dua maalumu kuliombea Taifa amani

Musoma. Waumini wa dini ya kiislamu mkoani Mara wamefanya dua maalumu kuliombea Taifa amani keuelekea uchaguzi mkuu, huku waumini hao wakitakiwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025. Dua hiyo imefanyika mjini Musoma leo Oktoba 25, 2025 katika Msikiti Mkubwa wa Ijumaa ambapo Sheikh wa Mkoa wa Mara, Kassim Msabaha amewataka waumini na Watanzania…

Read More

Sheria mpya ya uwekezaji kunusuru mashirika ya umma yasife

“Waziri kaniambia ile Sheria ya Msajili wa Hazina tayari imeshakamilika na iko tayari kusomwa kwa mara ya pili bungeni. Kwa hiyo naomba wabunge nendeni kaijadilini, mnapoona hapako vizuri turekebisheni, lakini ile sheria ipite ili apate mwongozo wa kumwongoza huyu (Msajili wa Hazina). “Lakini jingine, tuwe na uwezo sasa wa kuanzisha Mfuko wa Uwekezaji. Tutakapoanzisha Mfuko…

Read More

Dismas Nsindo ajitosa udiwani Kata ya Buyuni

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dismas Nsindo, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Kuwania Udiwani WA Kata ya Buyuni, wilayani Ilala, mkoani Dar es salaam. Nsindo ambaye ni mdau wa michezo, amechukua fomu hiyo katika Ofisi ya CCM Kata Buyuni, jijini Dar es Salaam  leo. Dirisha  la utoajia wa fomu Kwa wanachama ndani…

Read More

Daraja dogo la mbao chakavu lawatesa wanakijiji Hai

Hai. Wananchi wa Kijiji cha Kyuu, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kujenga daraja dogo katika eneo la Mto Kishenge, Kitongoji cha Maiputa, ili kuwawezesha kuendelea na shughuli mbalimbali za kijamii na kimaendeleo bila vikwazo. Ombi hilo limetolewa wakati wa ziara ya Ofisa Tarafa wa Masama, Nswajigwa Ndagile, alipotembelea eneo…

Read More

Dk Asha Rose – Migiro katibu mkuu mpya CCM

Dar es Salaam. Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imemteua Dk Asha Rose-Migiro kuwa katibu mkuu mpya wa chama hicho, kuchukua nafasi ya Dk Emmanuel Nchimbi ambaye ni mgombea mwenza wa urais wa CCM. Uteuzi wa Dk Migiro aliyewahi kuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), umetangazwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi…

Read More