Msikiti uliojengwa 1826 kuvunjwa kupisha ujenzi wa barabara Mbeya
Mbeya. “Historia inaenda kufutika”. Hiyo ni kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mbaraka Batenga, akielezea kuvunjwa kwa msikiti mkongwe uliopo mji mdogo wa Mbalizi wilayani Mbeya mkoani hapa. kupisha ujenzi wa barabara ya Mbalizi – Makongolosi. Msikiti huo ambao umedumu kwa miaka 198 tangu ulipojengwa mwaka 1826, umekuwa wa kihistoria na kivutio ambapo mbali…