Simbachawene ataka walioghushi barua za uhamisho kuchukuliwa hatua
Dodoma. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Simbachawene amezitaka mamlaka za nidhamu kuchukua hatua stahiki na kwa wakati kwa watumishi waliobainika kughushi barua na walioshiriki katika mchakato wa kughushi barua za uhamisho. Simbachawene ameyasema hayo leo Jumanne Desemba 17, 2024 wakati akifungua kikao kazi cha wakuu wa idara…