Malipo ya vyoo stendi kilio kila kona
Dar/Mikoani. Ni kilio kila kona, wananchi wakilalamikia tozo ya huduma ya choo inayokusanywa kwenye stendi kuu za mabasi za mikoa nchini. Ufuatiliaji uliofanywa na Mwananchi umebaini licha ya wananchi kuridhia malipo ya tozo ya kati ya Sh200 hadi Sh300 kwa huduma kwenye vyoo vya stendi, wanalalamikia tozo zingine wanazotozwa ili kuingia ndani ya maeneo hayo….