Miili miwili ya watu waliozama Ziwa Victoria yaopolewa
Mwanza. Miili ya watu wawili waliozama maji ndani ya Ziwa Victoria wakati wakitoka Kisiwa cha Yozu kusheherekea ‘Yanga Day’ kuelekea Kitongoji cha Itabagumba, Kata ya Burihaeke wilayani Sengerema imeopolewa. Miili hiyo ni miongoni mwa watu watano waliokuwa wakitafutwa baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria uliokuwa na watu 23 kuzama maji. Hata hivyo, watu 17 waliokolewa wakiwa…