WATUMISHI HOUSING YATOA ELIMU YA UWEKEZAJI NANENANE MBEYA

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Watumishi Housing Investments (WHI), ndugu Raphael Mwabuponde, ameendelea kutoa elimu kuhusu uwekezaji wa pamoja kupitia Mfuko wa Faida (Faida Fund) kwa wananchi na wanafunzi mbalimbali wanaotembelea maonyesho ya wakulima (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya. Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la WHI,…

Read More

Mwanzo, mwisho wa Papa Francis

Dar es Salaam. Alipochaguliwa kuwa Papa Jumatano Machi 13, 2013 akiwa na umri wa miaka 76, Papa Francis alikuwa na afya njema. Madaktari walisema tishu katika mapafu zilizoondolewa akiwa mdogo hazina athari kubwa kwa afya yake. Wasiwasi pekee ungekuwa kupungua kwa uwezo wa kupumua endapo angepata maambukizi ya njia ya hewa. Papa amekuwa akisumbuliwa na…

Read More

Kumi na moja wapenya mchujo wa mwisho uchaguzi TFF

KAMATI ya Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa orodha ya mwisho ya majina ya wagombea 11 waliopenya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa shirikia hilo uliopangwa kufanyika Agosti 16, 2025, jijini Tanga. Orodha hiyo ina majina ya wagombea 11 tu kati ya 25 waliojitokeza awali na kufyekwa kupitia hatua mbalimbali…

Read More

▪️Serikali kupunguza ada ya kodi ya pango kwa mwaka kwa Leseni ya chumvi ▪️Rais Samia apongezwa kwa kiwanda cha kusafisha chumvi Lindi ▪️Wazalishaji wa chumvi wafurahia kuanza kwa kodi ya zuio ▪️Serikali kudhibiti uingizaji wa chumvi kiholela nchini Dar es Salaam Katika kuwajengea uwezo wazalishaji wa chimvi nchini,Serikali imekuja na mikakati mbalimbali kufikia azma hiyo ikiwemo upunguzaji wa ada ya pango kwa mwaka ya leseni (Annual Rent) za uchimbaji mdogo wa chumvi nchini ili kusaidia kupunguza gharama za uzalishaji na kuchochea uzalishaji wa wingi wa chumvi nchini. Hayo yamesemwa jana tarehe 15 Julai, 2025 na Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga Kikao cha wadau wa sekta ndogo ya chumvi chini ya Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA). "*Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* ameendelea kutubeba sekta ya madini na wachimbaji kwa ujumla. Ni yeye aliyetuelekeza kusikilize kilio chenu na kutatua changamoto zinazowakabili ili mnufaike na shughuli mnazofanya" "Ametuelekeza Wizara ya Madini tuliridhie ombi lenu na kupunguza ada ya pango ya mwaka ya leseni ya uchimbaji mdogo kutoka Shilingi 45,000 mpaka Shilingi 20,000 kwa hekta, hili linakwenda kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza ubora wa chumvi ya mzalishaji mdogo" alieleza Mhe. Mavunde. Aidha, Waziri Mavunde alibainisha kuwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo udhibiti wa chumvi inayoingizwa kutoka nje ya nchi, zimepelekea bei ya chumvi ghafi kuongezeka na hivyo kuwanufaisha zaidi wazalishaji wadogo wa chumvi nchini. Uanzishwaji wa kodi ya zuio ya asilimia mbili (2%) kwenye mauzo ya chumvi ghafi kwa wazalishaji wenye leseni za PML imekuwa ni neema na manufaa kwao badala ya utaratibu wa awali wa kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato, ambao ulikuwa ni kero kubwa kwa wazalishaji wadogo. Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde alieleza kuwa Kiwanda cha kuzalisha chumvi cha STAMICO kipo hatua za mwisho, na kuagiza Shirika hilo kuhakikisha kabla ya mwezi wa Agosti kuisha kiwe kimekamilika na kuanza uzalishaji wa chumvi ili kupanua wigo wa soko la chumvi ya wazalishaji wadogo. Awali, akitoa taarifa ya utendaji wa Taasisi yao, Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA), Bi. Hawa Ghasia aliishukuru Serikali kwa kushughulikia changamoto zilizokuwa zinaikabili sekta ndogo ya chumvi nchini ambazo zimepelekea bei ya chumvi kupanda na kuwanufaisha zaidi wazalisha chumvi nchini.

▪️Serikali kupunguza ada ya kodi ya pango kwa mwaka kwa Leseni ya chumvi ▪️Rais Samia apongezwa kwa kiwanda cha kusafisha chumvi Lindi ▪️Wazalishaji wa chumvi wafurahia kuanza kwa kodi ya zuio ▪️Serikali kudhibiti uingizaji wa chumvi kiholela nchini Dar es Salaam Katika kuwajengea uwezo wazalishaji wa chimvi nchini,Serikali imekuja na mikakati mbalimbali kufikia azma hiyo…

Read More

Kipa Mzenji awataja Camara, Diarra

KIPA wa zamani wa Azam FC, Ahmed Salula anayeichezea Uhamiaji ya Zanzibar amesema makipa Djigui Diarra wa Yanga na Moussa Camara wa Simba ni chachu ya ushindani katika nafasi hiyo kwa wengine kutokana na viwango walivyo navyo vilivyowafanya kuaminiwa vikosini. Salula ambaye ni askari wa Jeshi la Uhamiaji, amesema anawafuatilia makipa hao wawili wa kigeni…

Read More