Mtibwa Sugar yapeleka mechi zake Jamhuri Dodoma
Kufuatia Uwanja wa Manungu Complex uliopo Morogoro kutokukidhi vigezo vinavyotakiwa ili utumike kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar imeuchagua Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kwa mechi za nyumbani za Ligi Kuu Bara. Mtibwa Sugar iliyorejea Ligi Kuu Bara msimu huu, imeanza kwa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mashujaa ikiwa ugenini. …