Watu zaidi ya 2000 wafukiwa na matope Papua New Guinea – DW – 27.05.2024
Sehemu kubwa ya kijiji cha Yambali kilichoko mkoa wa Enga ilifunikwa baada ya kuporomoka kwa mlima Mungalo majira ya asubuhi siku ya Ijumaa na kusomba majumba kadha na watu waliokuwa wamelala ndani yake. Kituo cha kusimamia majanga cha Papua New Guinea kimesema katika barua yake kwa Umoja wa Mataifa kwamba maporomoko hayo ya matope yalifukia zaidi…