Mlinzi aliyemuua muuza madini kunyongwa hadi kufa
Arusha. Mahakama ya Rufani imebariki adhabu ya kunyongwa hadi kufa, aliyekuwa mlinzi wa Kampuni ya la Commercial Coal Security Company, Edger Jackson, aliyemuua mfanyabiashara wa madini, Jofrey Mbepela. Edger alihukumiwa adhabu hiyo na Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Februari 9, 2023 kwa kumuua kwa kumpiga risasi mfanyabiashara akiwa mlinzi wa zamu ofisini kwa marehemu. Jopo…