
Tuungane pamoja tuimalize Morocco | Mwanaspoti
LEO ndiyo leo na asemaye kesho muongo, maana timu yetu ya taifa ‘Taifa Stars’ inaweza kuandika historia ya kibabe kwenye mashindano ya CHAN au safari yake ikaishia kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa itakapokabiliana na Morocco. Na kwa vile ni robo fainali, maana yake timu itakayopoteza itaaga rasmi mashindano hayo yanayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani…