Luvanga arejeshwa Twiga Stars | Mwanaspoti

BAADA ya kukaushiwa kwa muda mrefu, hatimaye mshambuliaji nyota wa timu ya soka ya wanawake ya  Al Nassr ya Saudi Arabia, Clara Luvanga amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 21 wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars kinachotarajia kushiriki mashindano maalumu. Clara aliyetwaa taji la Ligi Kuu ya Saudia akiwa na Al Nassr…

Read More

Balozi Bandora afariki dunia, kuzikwa Desemba 16

Dar es Salaam. Mwanadiplomasia nguli wa Tanzania, aliyewahi kuhudumu kama Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Mratibu Mkazi  wa Umoja wa Mataifa nchini Eswatini na Namibia, Timothy Bandora (72), amefariki dunia akiwa jijini Nairobi, nchini Kenya, ambako alikuwa akipatiwa matibabu. Bandora, ambaye aliitumikia Serikali kuanzia awamu ya kwanza hadi ya tatu, alitekeleza majukumu mbalimbali ya…

Read More

Beno aukubali mziki wa Mgunda

KIPA wa Namungo FC, Beno Kakolanya ameuzungumzia ujio wa kocha mpya, Juma Mgunda katika kikosi hicho akisema umeongeza mzuka kwa wachezaji kwani nje ya taaluma yake anasimama kama baba na anaamini muda si mrefu timu hiyo itarejesha makali yaliyozoeleka Bara. Kakolanya alisema amefanya kazi na Mgunda akiwa Simba na sasa amekutana tena Namungo, hivyo anamfahamu…

Read More

Kibwana bado yupo yupo sana

UONGOZI wa klabu ya Yanga, umemuongeza mkataba wa miaka miwili beki wao wa kulia, Kibwana Shomari kuendelea kuitumikia klabu hiyo. Kibwana ambaye ameitumikia Yanga kwa miaka mitatu tangu ametua akitokea Mtibwa Sugar, ataendelea kubaki zaidi ndani ya timu hiyo ya Jangwani kwa miaka mingine miwili. Beki huyo ambaye ametwaa mataji mawili ya Ligi Kuu Bara…

Read More

WADAU WA MADINI WAPIGWA MSASA DODOMA

Tume ya Madini inaendelea kutoa elimu kwa wadau wa madini na wananchi wote kutoka katika Mkoa wa Dodoma kwenye Wiki ya Maonesho ya Madini inayoambatana na Kongamano la Wachimbaji wa Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Kikwete, leo tarehe 22 Juni 2024, Dodoma. Elimu inatolewa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji…

Read More

Sh6.7 bilioni kupunguza msongamano wa wajawazito Kahama

Kahama. Idadi ya watoto wanaozaliwa katika Hospitali ya manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga kwa siku ni 20 hadi 25, kwa mwezi ni watoto 675, jambo ambalo limetajwa kusababisha msongamano mkubwa kwenye wodi ya mama na mtoto hospitalini hapo. Kutokana na hali hiyo akina mama wanaojifungua watoto njiti kwenye hospitali hiyo wanakosa sehemu yenye stara kwa…

Read More