Papa Leo XIV kuwekwa wakfu kuliongoza kanisa, vigogo duniani wahudhuria
Roma. Ibada rasmi ya kuwekwa wakfu kwa Papa Leo wa XIV, papa wa kwanza kutoka Marekani, inaendelea katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, ikihudhuriwa na viongozi wa dunia, familia za kifalme, na maelfu ya waumini. Papa huyo wa 267, aliwasili mjini Vatican kwa kutumia gari maalumu la kipapa (popemobile) na kupokelewa kwa shangwe na umati mkubwa…