Hali tete maelfu wakimbia DRC, raia wasota kutafuta hifadhi
Dar es Salaam. Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeingia tena katika taswira mpya ya machafuko, ikiwa ni mfululizo wa miaka mingi ya ghasia ambazo zimelifanya eneo hilo kuwa kitovu cha vita visivyokoma. Mashambulizi ya waasi wa M23 yameibuka tena yakishika kasi katika hali inayovuruga makubaliano ya amani yaliyofanyika wiki iliyopita yakipewa matumaini…