Rais Samia avunja bodi ya NSSF, afanya uteuzi
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameivunja bodi ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuwateuwa watendaji mbalimbali. Bodi ya NSSF ilikuwa inaundwa na Mwenyekiti wake, Mwamini Malemi, Makamu, Abdul Zuberi, huku wajumbe ni Juliana Mpanduji, Joseph Nganga, John Kinuno, Henry Mkunda, Fauzia Malik, Lucy Chigudulu na Oscar Mgaya….