
Huu hapa utaratibu kuomba ufadhili masomo ya ubingwa bobezi wa afya
Dodoma. Serikali imeendelea kuwekeza kwa kwenye sekta ya afya kupitia mpango wa ufadhili wa masomo Samia Health Super-Specialization Program, ambapo kwa mwaka wa fedha 2025/26 imetenga Sh9 bilioni kugharamia ufadhili wa mafunzo ya ubingwa na ubingwa bobezi kwa wataalamu wa afya. Hayo yamebainishwa leo Alhamisi Agosti 21, 2025 na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, wakati…