Wanaodaiwa kumteka Mtanzania Kenya wasota mahabusu siku 16
Dar/Nairobi. Mahakama nchini Kenya, kesho itatoa uamuzi wa iwapo raia wawili wa Kenya na Mtanzania wanaotuhumiwa kufanya jaribio la kumteka mwanaharakati wa Tanzania, Mshabaha Hamza, waachiwe kwa dhamana ama la. Katika jaribio hilo la utekaji ambalo lilishindikana, lililotokea Februari 22, 2026 huko Kaunti ya Machakos katika ardhi ya Kenya, watuhumiwa wanadaiwa kumchoma sindano mwanaharakati huyo…