HISIA ZANGU: Pamba karibuni katika ufalme wa Aziz KI, Chama
RAFIKI zetu wa Mwanza Pamba wamerudi Ligi Kuu. Imepita miaka 22 tangu walipoondoka zao. Umri wa mtu mzima. Nyakati zimekwenda wapi? Hatujui. Walikuwa na shangwe kwelikweli katika mitaa yao. Namna walivyopokewa ungeweza kudhani wametoka kutwaa Kombe la Dunia. Unaikumbuka Pamba halisi? Wakati huo wakiwa na kina Fumo Felician, Khalfan Ngassa baba yake Mrisho Ngassa, Kitwana…