MILIONI 300 KUKAMILISHA UJENZI JENGO LA KUHIFADHIA MAITI HOSPILI YA RUFAA MKOA WA KATAVI
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la kuhifadhia Maiti Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Katavi. Kauli hiyo imebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel leo Jijini Dodoma wakati akijibu swali Namba 254 kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Taska Restituta…