Hidaya chapoteza nguvu baada ya kuingia Mafia
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kupitia mwendelezo wa taarifa zake kuhusu kimbunga Hidaya imesema kimekosa nguvu baada ya kuingia nchi kavu katika Kisiwa cha Mafia. Taarifa hiyo imetolewa jana Jumamosi Mei 4, 2024 saa 5.59 usiku. “Taarifa hii inahitimisha mfululizo wa taarifa wa kilichokuwa kimbunga Hidaya zilizokuwa zikitolewa na TMA…